Tuesday, June 16, 2015

Anonymous

BARNABA Aitumia Vizuri Changamoto ya Kukosa Tuzo, Atangaza Mipango Yake Mwaka Huu!

Muimbaji na muandishi wa nyimbo, Barnaba baada ya kukosa tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka- Bongo Fleva kwenye KTMA 2015, ameitumia kama changamoto na kutangaza kutoa album mwaka huu ili kuwafanya hata wale ambao hawakumuelewa wamuelewe zaidi.
Barnaba
Barnaba alitumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru mashabiki waliompigia kura pamoja na wasanii wenzake aliokuwa akiwania nao kipengele kimoja, na mwisho kuweka ahadi ya kutoa album. 

Hiki ndicho alichokiandika:
“Nawashukuru watu wangu wote na mashabiki Zangu mlionipiga Kura naamini kila kilichotokea Kimestahiri Kutokana Mimi nampenda mungu na naamini kuna Kitu kinaitwa Wakati au muda na napenda Changamoto mana hii Itafanya Nifanye Vyema mara mbili ya pale ninapofanyaga Yes Of coz mimi sinaga Team Bali Team yangu ni wale wote wanaopenda Muziki Mzuri nawapenda wote na nawapa Ongera wenzangu wote mlioshinda Bila kusahau kipenzi Changu #bestfemaleperformer and #bestfemaleartist @Vanessamdee Kushinda kwako ni wazi inaonesha wazi kazi nzuri Aya Tunaendelea na kazi Ya kuangusha Vyuma Juu Ya Vyuma na mwaka Huu natoa #Album Ambayo itafanya Yule asiyemwelewa Barnaba ajue na aelewe mwisho nawakumbusha Umoja ni nguvu utengano…………. Tusijenge Matabaka Nndugu zangu”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.