Wilbert Molandi, Dar es Salaam
KIUNGO mpya wa Yanga, Geofrey Mwashiuya, hadi hivi sasa ndiye mchezaji aliyeng’ara kwenye mazoezi ya timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.
Mwashiuya alisajiliwa na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo la msimu uliopita, lakini alishindwa kuonekana uwanjani kuonyesha makali yake kutokana na timu yake ya Kimondo kudai bado ina mkataba naye.Hivyo, kiungo huyo anatarajiwa kuanza kuonekana kwenye msimu ujao wa wa ligi kuu baada ya Yanga kumalizana na Kimondo iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Katika mazoezi hayo, yaliyofikia siku saba tangu yameanza, kiungo huyo ndiye aliyeonyesha uwezo mkubwa ndani ya uwanja kushinda wakongwe aliowakuta.Kwa kuanzia kwenye pumzi, kiungo huyo ameonekana kuwa na pumzi nyingi katika kukimbia mbio ndefu na fupi, akifuatiwa na Msierra Leone, Lansana Kamara.
Achana na pumzi, ameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao ya mita 20 kwa kupiga mashuti makali yanayowashinda makipa, Ally Mustapha ‘Barthez’ na Benedicto Tinoco aliyetua kuichezea Yanga hivi karibuni akisaini mkataba wa miaka mitatu.
Katika mazoezi ya jana, kiungo huyo alifanikiwa kufunga bao pekee kwa njia ya shuti kali ndani ya 18 akimfunga Barthez akiunganisha pasi ya Kamara.
Pia, kiungo huyo aligongesha mwamba wa goli mara tatu kwa kupiga mashuti matatu makali yote ya mita 20.
Gumzo kubwa kwa mashabiki wa Yanga ni kiwango cha hali ya juu ambacho amekuwa akionyesha kiungo huyo kila kukicha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.