Mwenyewe afunguka, aitaja Simba
HALI ya mambo ipo kwenye kiza juu ya usajili wa kiungo Lansana Kamara katika kikosi cha Yanga baada ya kubainika kuwa kuna hatihati ya kutoitumikia timu hiyo msimu ujao kwa kile kilichoelezwa kwamba benchi la ufundi la timu hiyo halijaridhishwa na kiwango chake.
Kamara, raia wa Sierra Leone, yupo nchini akisikilizia dili la kutua Yanga na alianza mazoezi chini ya Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, wiki iliyopita lakini pia mchezaji huyo akafunguka na kuzitaja Simba na Azam FC.
Mtu wa ndani wa Yanga, amelidokeza Championi Ijumaa kuwa, uwezo wa kiungo huyo bado haujamkuna Pluijm na jopo lake la ufundi, hivyo anaweza kuachwa kwa kuwa kocha huyo lengo lake ni kutafuta mchezaji mwenye kiwango cha juu kuliko waliopo.
“Siyo kwamba Kamara ni mbaya, yupo vizuri ila sasa suala linakuja kwamba anaonekana amezidiwa baadhi ya vitu na viungo aliowakuta hapa, ingawa bado Pluijm anataka kuendelea kumuangalia zaidi kabla ya kutoa maamuzi na amewekewa kipimo cha mwisho katika mechi za kirafiki kabla ya kuanza ligi,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipoulizwa juu ya mchezaji huyo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, alisema: “Tutamuangalia kwenye mechi za kirafiki za hivi karibuni na baada ya hapo ndiyo tutakuwa na lolote la kusema juu yake, kama tutamsajili au vipi.”
Upande wa Pluijm naye alifunguka: “Hapana, siwezi kukwambia chochote kwa sababu bado ninamuangalia na tunahitaji kumuangalia zaidi, tusubiri kwanza nimuone kwenye mechi.”
Wakati huohuo, Kamara aliliambia gazeti hili kuwa tayari ameshawaambiwa juu ya wapinzani wakubwa wa Yanga, ambao ni Simba na Azam. “Sijui vizuri soka la Tanzania, lakini nimeambiwa kuwa wapinzani wakubwa sana wa Yanga ni Simba na Azam, ninatamani sana kucheza dhidi ya timu hizo kwa kuwa ninapenda changamoto katika maisha ya soka,” alisema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.