Monday, June 1, 2015

Anonymous

SENTENSI 23 MUHIMU ZA MH. MWIGULU NCHEMBA AKITANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS TANZANIA

  1. Mwigulu: Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha leo kusimama mbele yenu kwaajili ya kutangaza jambo kubwa kwa ajili ya nchi yetu. 
  2. Mwigulu: Nimeamua kutangazia nia Dodoma kwakuwa ni Makao makuu ya Nchi na pia makao makuu ya chama. 
  3. Mwigulu: Nilipomaliza shahada ya 2 nilibeba zege na mke wangu alipika mama ntilie, natambua tatizo la ajira kwa vijana. 
  4. Mwigulu: Kukaa sana serikalini si kigezo, unaweza kukaa sana serikalini na ukawa umesababishia hasara kubwa Taifa hili 
  5. Mwigulu: Kiongozi akipatikana kwa mazoea, atafanya kazi kwa mazoea. Nawaambieni tunataka tukomeshe kufanya kazi kwa mazoea. 
  6. Mwigulu: Unafanya kazi ukiwa na nguvu na ukimaliza unapumzika, kwahiyo unajiuliza tena hilo? 
  7. Mwigulu: Mkataba wa Rais wa awamu ya tano ni juu kazi anazoenda kufanya na sio kazi alizowahi kufanya. 
  8. Mwigulu:Mambo ya kuzingatia ni Kila mtu kulipa kodi anayostahili na sio kukandamiza wafanyakazi na kinamama wauza vitumbua. 
  9. Mwigulu: Pia jambo lingine la kuzingatia ni Udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. 
  10. Mwigulu: Awamu ya 5 nataka kuona nchi ikiingia kwenye uchumi wa viwanda na vijana wakifanya kazi kwa shift usiku na mchana. 
  11. Mwigulu: Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na rushwa hurudisha nyuma maendeleo 
  12. Mwigulu: Mtu yoyote akithibitika amefanya vitendo vya rushwa, atafilisiwa, atafukuzwa kazi na atafungwa. 
  13. Mwigulu: Mtu anabakiza muda mchache hadi anakuja kustaafu unamuongezea muda tena kazini wakati kuna vijana wasio na kazi. 
  14. Mwigulu: Ninaposema kukomesha rushwa nitazingatia maslahi ya Wafanyakazi, haiwezekani wengine Wale kidogo na wengine kubwa. 
  15. Mwigulu: Mtu anayeiba dawa ambazo zingemtibu maskini huyo ni mhujumu, tutamnyang'anya leseni yake na atakwenda jela. 
  16. Mwigulu: Tutasimamia Muungano wetu maana sio wa vitu ila ni watu. tutahakikisha uchumi wa Zanzibar nao utapewa kipaumbele. 
  17. Mwigulu: Nawaambieni nawaomba kazi hii nikiwa bado nina nguvu ili niweze kufika mwenyewe maeneo yenye migogoro ya ardhi. 
  18. Mwigulu: Ninapotangaza nia ya jambo hili nimetathimini vya kutosha na nikajiridhisha na ahadi yangu ni kwamba nitawavusha. 
  19. Mwigulu: Tunaposimamia kuacha kufanya kazi kwa mazoea ndio tunasema mabadiliko ni vitendo na wakati ni sasa 
  20. Mwigulu: Ukiwaondoa vijana mjini wakati wakifanya kazi halali kwa kigezo cha uchafu,watarudi mjini na kufanya kazi haramu 
  21. Mwigulu: Natangaza rasmi kuomba ridhaa ya kugombea katika chama changu ili niweze kuleta mabadiliko Katika Nchi yangu. 
  22. Mwigulu: Napoenda kupigana vita hii siendi kupigana kwaajili ya Watanzania ila mimi mwenyewe maana umaskini unanigusa.  
  23. Mwigulu: Mambo matatu ninayowaomba Watanzania ni kwamba mniamini, pili mniunge mkono na tatu nitawavusha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.