USIKU wa kuamkia leo kulikuwa na bonge la shoo
lililokuwa likienda kwa jina la Gossip Night Party ndani ya ukumbi wa
Bills uliopo Posta jijini Dar es Salaam, ambapo wasanii kibao wa muziki
wa kizazi kipya walipata fursa ya kufanya makamuzi huku wakitumia muda
huo kumuenzi msanii mwenzao Albert Mangwea ambaye alifariki miaka miwili
iliyopita.
Wasanii waliopata fursa ya kufanya makamuzi kwenye shoo hiyo ni
pamoja na Godzillah, Baraka Da prince, Abdul Kiba, Chid Benz, Shilole,
Barnaba na wengine kibao.
(Habari Picha: Musa Mateja/GPL)

Note: Only a member of this blog may post a comment.