MKONGWE wa filamu za mapigano kutoka Hollywood,
Dolph Lundgren hivi karibuni alijikuta katika wakati mgumu baada ya staa
mwenzake wa kituo cha MTV, Matthew Pritchard kumkojolea akiwa ndani ya
ndege.
Matthew akiwa katika harakati za kumkojolea Dolph (aliyezungushiwa duara).
Tukio hilo lilitokea ndani ya ndege binafsi iliyobeba mastaa hao
wakiwa na watu wengine wengi ambapo Dolph pamoja na watu hao walikuwa
wakitokea jiji la Amsterdam, Uholanzi kwenda Marekani kuhudhuria
mashindano ya mbio za magari yajulikanao kama Gumball 3000 ambayo
hufanyika Reno, Nevada.
Inasemekana kuwa Matthew alikuwa akinywa kilevi kilichochanganywa na
vidonge vya kulevya vijulikanavyo kama Xanax na kumpelekea kuvua nguo
zote na kupanda juu ya siti ya ndege na kuanza kucheza wakati ndege hiyo
ikitua katika bandari ya mji mkuu huko Uholanzi.
Matthew akiwa amesinzia baada ya kunywa vidonge hivyo.
Baada ya picha na vipande vya video hizo kusambaa katika mtandao ya
kijamii, Facebook, Matthew alivunja ukimya na kusema;“Nilichukua Xanax
ambayo niliamini itanifanya nilale nikiwa ndani ya ndege.
“Sikujua kama itakuwa na madhara kama ikichanganywa na kilevi.
Nilikuwa nina kilevi sana mwilini. Nikaanza kukimbia nikiwa ndani ya
ndege utupu. Nikaanza kumkojolea Dolph miguuni mwake.
“Baada ya hapo, Dolph alinishika mikono yangu na kuniambia nisijali
kwa hili lililotokea. Sijui hata ni kwanini sikuadhibiwa pale uwanja wa
ndege.“Nilimuomba msamaha@dolphlundren na amepokea msamaha wangu kama
mtu mtanashati,” aliandika Matthew kwenye ukurasa wake wa Twitter.
(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL)

Note: Only a member of this blog may post a comment.