Wilbert Molandi, Dar es Salaam
NIMEKUJIBU! Hivyo ndivyo utakavyoweza kutamka kwa mshambuliaji mpya mkongwe wa Simba, Mussa Mgosi baada ya kumjibu kiungo mshambuliaji wa Free State FC ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa kwa kununua mkoko aina ya Volkswagen March.

Mshambuliaji huyo, hiyo ni gari ya tatu anayomiliki, nyingine zikiwa ni Toyota Opa na Noah. Volkswagen hiyo ina rangi ya silva na amekuwa akitanua nayo mitaa mbalimbali jijini Dar.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mgosi alisema kuanzia hivi sasa na mara nyingi atakuwa anaonekana anatanua na mkoko huo baada ya kuuvuta hivi karibuni.Mgosi alisema, hiyo yote ni katika kurahisisha maisha yake, kikubwa anataka kuona anakuwa tofauti na wenzake, hivyo haoni sababu ya yeye kushindwa kumiliki gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni 25.” alisema Mgosi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.