Wednesday, June 17, 2015

Anonymous

Kaseke atua YANGA SC, Pluijm ampeleka shule!

Wilbert Molandi,Dar es Salaam
AKITUA kwa mara ya kwanza kujiunga na Yanga, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Deus Kaseke, aliwekwa kitimoto na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

Kiungo huyo, alijiunga na kikosi hicho hivi karibuni akasaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo akitokea Mbeya City baada ya mkataba wa kuichezea timu hiyo kumalizika.Kwa mara ya kwanza, kiungo huyo aliripoti jana Jumanne asubuhi kwenye mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Pluijm alionekana kama vile anampeleka darasani kiungo huyo mara baada ya mazoezi kumalizika akiwa na msaidizi wake Charles Mkwasa kutokana na kuonekana kushindwa mambo mengi waliyokuwa wanataka.

Pluijm na Charles Boniface Mkwasa walikaa katikati ya Uwanja wa Karume na kiungo huyo kwa zaidi ya dakika 20 huku makocha hao wakionekana wakimuonyesha jinsi ya kupiga pasi, kupokea mpira, kukimbia na kupiga vichwa.
Katika mazungumzo hayo, kocha huyo alionekana akimpa maelekezo mbalimbali Kaseke kwa njia ya vitendo akitumia mikono na miguu yake.

Wakati akipewa maelekezo hayo, kiungo huyo alionekana akiitikia kwa kutingisha kichwa huku Mkwasa akimuelekeza baadhi ya vitu.Katika mazoezi ya jana asubuhi, kocha huyo aliwapa programu tano ikiwemo ya kukimbia mbio fupi, ndefu kabla ya kupanga vikosi viwili kucheza mechi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.