Mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa Mtanzania
amekamatwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 75 katika Uwanja wa
Ndege India ambapo mwanamke huyo alikamatwa akiwa na hati ya kusafiria
ya Tanzania.
Mwanamke huyo alikamatwa katika Uwanja
huo ambapo aligundulika kubeba mzigo huo baada ya mbwa kunusa mizigo
yake akiwa eneo la upekuzi.
Milind Lanjewar ambaye
ni Ofisa wa Uwanja huo amesema hicho ni kiwango kikubwa zaidi cha dawa
za kulevya kukamatwa katika kipindi cha hivi karibuni.
Lanjewar amesema mwanamke huyo alikuwa na mzigo wa unga ambao ni dawa za kulevya aina ya Methaqualone au Mandrax na Cocaine.


Note: Only a member of this blog may post a comment.