Thursday, June 4, 2015

Anonymous

KUMEKUCHA! MHESHIMIWA SUGU APATA MPINZANI UBUNGE MBEYA MJINI...NI MSANII WA BONGO MUVI!

KUMEKUCHA! Nyota wa sinema za Kibongo, Jimmy Mafufu ameibuka na kuwa msanii wa kwanza kutangaza nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nyota wa sinema za Kibongo, Jimmy Mafufu.
Akipiga stori na safu hii juzi jijini Dar, Mafufu alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuombwa na wananchi wa jimbo hilo kwa vile mbunge wa sasa, Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hajatimiza ahadi zake.
“Nakwenda Mbeya, Ijumaa (kesho) nitatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe, nitapokelewa pale na wana-CCM tayari kwa kuanza mchakato wa kuchukua fomu kwa tiketi ya CCM kugombea ubunge. Ni mimi tu ndiye nitakayeiweza Mbeya Mjini,” alisema Mafufu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.