Bondia wa Marekani, Floyd Mayweather anatarajia kuongeza orodha ya
magari ya kifahari anayomiliki kwa kununua ndinga yenye thamani ya dola
milioni 4.8.
Floyd ataumwaga mkwanja huo kununua gari aina ya Koenigsegg CCXR Trevita, ambazo zipo tatu tu duniani.
Ataiongeza gari hiyo kwenye magari yake yenye thamani ya dola milioni
55 yakiwemo Ferrari, Porsche, Lamborghini, Bugatti na ndege binafsi
yenye thamani ya dola milioni 30.
Mwaka huu bondia huyo ameshika nafasi ya kwanza ya mwanamichezo aliyeingiza fedha nyingi zaidi duniani kwa kutengeneza mkwanja wa dola milioni 300.
Mwaka huu bondia huyo ameshika nafasi ya kwanza ya mwanamichezo aliyeingiza fedha nyingi zaidi duniani kwa kutengeneza mkwanja wa dola milioni 300.
Fedha hizo aliingiza May 2 baada ya kuzichapa na Manny Pacquiao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.