JACOB Steven Mbura ‘JB’ anaendelea na simulizi yake tamu ya safari ya maisha, tangu kuzaliwa, makuzi, malezi na kila hatua alizopita katika maisha yake hadi kufika alipo leo. Ni simulizi isiyochosha masikioni! Imejaa kila aina ya vimbwanga, matukio ya kushangaza na wakati mwingine masikitiko.
Tuko sehemu ya tano sasa, wiki iliyopita aliishia pale alipoyakumbuka maisha matamu aliyoishi jeshini, licha ya kukumbana na changamoto nyingi, lakini hakusahau utamu wa kampani aliyokuwa nayo!
Ilifika mahali uzalendo ulimshinda, kumbukumbu zikamuelemea na kujikuta akimwaga machozi! Je, nini kilifuata?
SHUKA NAYO MWENYEWE…
“Ngoja nikuoneshe kitu mdogo wangu,” alisema JB huku akichukua simu yake kubwa na ya gharama, akawa ananionesha picha za baadhi ya watu ambao ni viongozi wa ngazi za juu mno serikalini, ambao walikuwa pamoja jeshini, Kabuku Tanga na msanii huyu.
“Haa…na huyu ulikuwa naye jeshini?” nilimuuliza JB baada ya kuona picha ya mtu ambaye hata wewe msomaji ukimjua, siyo rahisi kuamini kama aliwahi kuwa jeshini na JB.
“We acha tu mdogo wangu, ndiyo maana ninaposimulia kumbukumbu ya maisha yangu, hususan jeshini, nashindwa kuyazuia machozi,” anasema huku akiendelea kunionesha picha za viongozi wengine ambao msanii huyu alipata nao mafunzo ya jeshi.
“Mmh, kaka ikawaje?” nilimuuliza nikimtaka aendelee na simulizi.
“Kwa hiyo nikiwa jeshini nilipitia vitengo mbalimbali. Moja kati ya vitengo vigumu nilivyovipitia jeshini ni ubaharia,” anasema JB huku akitabasamu na kunitazama usoni kwa muda.
“Ubaharia jeshini?” nilimuuliza.
“Nilijua ni lazima ushangae kusikia ubaharia jeshini. Sikiliza, kwa waliopita jeshini wanajua maana ya neno ubaharia,” alisema.“Ubaharia ni upishi, kule jeshini mtu anayefanya kazi ya upishi, huitwa Baharia,” anasema JB na kuendelea;
“Kwa hiyo nikawa mpishi wa kambi, lakini upishi wenyewe siyo kama unavyodhani, sikiliza,” alisema JB lakini safari hii kwa sauti ya juu na kuwafanya baadhi ya watu waliokuwa karibu kugeuka na kututazama kwa muda.
“Unakuta sufuria ni kubwa mno, halafu mwiko mkubwa kwa hiyo unakuwa unalitupia limwiko huku, kule na kuufinyanga ugali kwa kuupiga na mwiko yaani hivi, hivi, hivi, hahahaha….,” anasema JB huku akitolea mfano wa jinsi alivyokuwa akipika kabla ya kumalizia maelezo hayo kwa kicheko!
“Mmh, ikawaje?” nilimuuliza nikiwa ‘siriazi’ kidogo.
“Basi bwana, baadaye nilihamia kitengo cha kwata za kawaida na maeneo mengine ya kijeshi kambini hapo,” anasema JB.
NINI TOAFUTI YA MAISHA YA JESHINI NA URAIANI?
“Unajua jeshini hakuna uhuru mkubwa kama huku uraiani, nadhani siyo jeshini tu, kila mahali palipo na taasisi fulani, hapawezi kuwa na uhuru kama uraiani, maana kuna sheria za kuzingatiwa, huwezi kujiachia kwa kujiamulia mambo kama huku uraiani,” anaweka bayana JB.
JB anasema, kwa muda wa mwaka mzima alioutumia kuwa jeshini, alijifunza mambo mengi mno ambayo kwa hakika yanamsaidia maishani hadi sasa. Anasema kila anapokumbana na vikwazo vya kimaisha, amekuwa akitumia uzoefu wake jeshini wa namna ambavyo walijifunza kukabiliana na changamoto za kimaisha.
“Mambo niliyojifunza jeshini, hakika yananisaidia mno hadi sasa, jeshi ni zuri mno, naishukuru sana serikali kwa kurejesha utaratibu wa watu wanaohitimu masomo ya kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya kijeshi, ni jambo jema,” anasema JB.
NI TUKIO GANI LA AJABU ANALOLIKUMBUKA JESHINI?
“Aaah, sitasahau siku ambayo nili…
Usikose wiki ijayo!

Note: Only a member of this blog may post a comment.