Natumaini utakuwa u-mzima wa afya kabisa. Kwa wiki kama nne mfululizo tumekuwa tukiangalia juu ya tatizo la wanawake wengi kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Tumeangalia sababu za tatizo hilo na tukaangalia athari zake na wiki iliyopita na kujifunza njia za kutatua tatizo hilo.
Kama ilivyo matatizo mengine tatizo la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa huwakumba na wanaume vilevile ila siyo kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwa wanawake.Katika makala haya tutaaangalia kwa kina sababu za tatizo hili kwa wanaume na athari zake na mwisho tutajifunza njia za kutatua au kuondokana na tatizo hili.
Mwili wa mwanadamu uliumbwa ukiwa na matamanio na matamanio haya si mabaya kama mwenye mwili atakuwa na uwezo wa kujitawala. Wanaume wengi huvutiwa zaidi na hisia za kushiriki tendo kwa kuona baadhi ya maungo kwa wanawake, kusikia sauti na hata migusano.
Kuna wanaume wengi wao wapo tu siku zinaenda hawapati hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wanajiona kama ndio wamefanikiwa kujitawala kumbe ni wagonjwa.
Habari njema ni kwamba pamoja na tatizo hili kuwasumbua watu wengi kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa, kwa kutumia mimea tiba na matunda tiba. Unachotakiwa kufanya kama umejaribu kutumia njia mbalimbali ili kuondoa tatizo hili bila mafanikio basi wahi mapema kwa wataalamu ufanyiwe uchunguzi au ukatutembelea Sigwa Herbal Clinic tukakusaidia kuliondoa kabisa tatizo hilo. Baadhi ya watu wanamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadiri umri wa mwanaume unavyoongezeka.
Kuna idadi kubwa tu ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa. Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa tatizo hili. Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake. Hata hivyo tatizo la mwanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo limekuwa ni chanzo kikubwa katika kuleta migogoro katika ndoa nyingi.
Kwa kawaida wanaume ni wabishi sana na huwa hawapendi kuaibika hivyo mtu anaweza akawa na tatizo ila hapendi mwenzi wake ajue kama ana tatizo ambalo kumbe angeliweka bayana angepata ushauri wa namna ya kulitatua.
Pamoja na kwamba tatizo hili halijitokezi sana kwa wanaume ukilinganisha na wanawake, inakadiriwa kuwa asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wana tatizo hili, ni sawa na uwiano wa mwanaume mmoja kwa kila wanaume sita au saba. Idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni mara mbili ya wanaume. Tatizo hili huwakera zaidi wanaume kuliko wanawake kwa sababu wanaume huchukulia ulijali kama sehemu ya ukamilifu wa mwanamme na hukosa raha wanapoona wana upungufu kuhusu mambo ya mapenzi, tofauti kabisa na wanawake.
Nakushauri msomaji wangu ufuatilie kwa makini makala haya ili kujua vizuri kuhusu tatizo hili. Lakini kama una tatizo hili na unajisikia aibu kumweleza mwenzi wako tupigie simu katika namba zetu au tutembelee Sigwa Herbal Clinic katika vituo vyetu vilivyopo Dar es Salaam, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha, Tanga, Kigoma, Mwanza.
Saturday, June 20, 2015
JIFUNZE HAPA! KWA NINI WANAWAKE WENGI WANAKOSA HAMU YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA?-5
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
MAPENZI
on Saturday, June 20, 2015

Note: Only a member of this blog may post a comment.