Nyota za vijana wa Yamoto Band inaendelea kung’ara, baada ya kushoot
video na Godfather Afrika Kusini wiki chache zilizopita, vijana hao
wamepata mwaliko wa kwenda kuwaburudisha Watanzania na wana Afrika
mashariki waishio Marekani.
Mkubwa Fella ameiambia Bongo5 kuwa mwaliko huo wameupata siku chache zilizopita kutoka kwa Watanzania waishio huko.
“Mpaka sasa hivi watafanya show miji miwili lakini Minnesota nao
wametaka halafu na New Jersey kuna Watanzania wanaoishi kule nao
wamehitaji, lakini mpaka sasa hivi waliotuletea mikataba ni sehemu mbili
ila kuanzia jana watu wengi nao wametaka madogo waende.” Alisema Fella.
Show ya kwanza itafanyika Novemba 28, 2015 huko Houston Texas, ikifatiwa na show ya pili Desemba 5, 2015- Washington DC.
Mmoja wa mapromota wa Marekani alipost kuhusu ziara ya Yamoto band Marekani:

Mwaka 2015 umekuwa na mafanikio kwa Yamoto kimataifa, miezi michache
iliyopita waimbaji hao wa ‘Ntakupwelepweta’ walitumbuiza nchini
Uingereza pamoja na Muscat.
Fella ameongeza kuwa Video mpya walioyoshoot Afrika Kusini itatoka baada ya Ramadhan.
-via bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.