Monday, June 1, 2015

Anonymous

GOOD NEWS: MUIGIZAJI NYOTA TONTO DIKEH KUOLEWA HIVI KARIBUNI

Staa wa filamu za Kinigeria, Tonto Dikeh.
Lagos, Nigeria
STAA wa filamu za Kinigeria, Tonto Dikeh, 29, amevunja ukimya baada ya kusema ataolewa hivi karibuni na mchumba wake, Churchill Olakunke Oladunni a.k.a Mr. X ambaye ni mfanyabiashara.

Staa wa filamu za Kinigeria, Tonto Dikeh akiwa na mpenzi wake Churchill Olakunke Oladunni a.k.a Mr. X.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa tayari mume huyo mtarajiwa aliwahi kumuoa Bimbo Coker mwaka 2012 na haijawekwa wazi kama waliachana na mkewe huyo.Tonto alifunguka hayo kwenye mahojiano maalumu na chombo kimoja cha habari nchini hapa. 

Staa huyo aliulizwa kuhusiana na pete aliyokuwa amevaa kama amechumbiwa, awali alijibaraguza akitaka kuchengesha swali hilo, kabla ya mwandishi kumkazia akitaka amjibu ndipo binti akaamua kufunguka kuwa ni kweli na ataolewa hivi karibuni. “Una macho makini, ndiyo nitaolewa,” alisema Tonto kwa kifupi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.