Ndoto za vijana waliotegenezwa na Mkubwa Fella, Yamoto Band za kwenda
kimataifa zinaelekea kutimia. Vijana hao wamewasili jana nchini Afrika
Kusini, ambako wameenda kushoot video yao ya kwanza kuwahi kufanya na
director mkubwa wa nje.
Yamoto wameshare picha wakiwa Afrika Kusini na uongozi wao, Said
Fella, Babu Tale na Diamond. Katika picha hizo walionekana wakiwa kwenye
kikao na director atakayefanya video yao Godfather.
“Hii ni mipango ya video jinsi itavyokuwa yani jinsi gan itaanza
na itaisha asante mungu asante pia@mkubwafella @babutale
@diamondplatnumz@i_am_godfather dua zenu 2 wadau amen.” aliandika muimbaji wa band hiyo Beka kwenye moja ya picha hizo.
“Mikakati inaanza na @i_am_godfather na vijanaa wa @yamoto_band
kuhusu video kesho na kaka yao @diamondplatnumz mungu tushikie wajawako
na hili” Aliandika Babu Tale

Note: Only a member of this blog may post a comment.