Wiki moja baada ya ofa ya kwanza ya Manchester United kumsajili
Sergio Ramos kukataliwa na Real Madrid, hatimaye mchezaji huyo ambaye
yupo mapumzikoni ametoa kauli yake.
United
walituma ofa ya kwanza ya paundi millioni 28.3 kwa Madrid ili kupata
saini ya beki huyo wa kimataifa wa Spain, lakini Madrid waliikata ofa
hiyo.
Hata hivyo baada ya Ramos kugundua Madrid wameikataa ofa hiyo,
alichukua uamuzi wa kuwaweka wazi viongozi wa Madrid kupitia wakala wake
kwamba – Anataka kuondoka na kujiunga na United na kuiomba Madrid
ikubaliane bei na Manchester United.
Madrid wanategemewa kujaribu kumtuliza Ramos na mkataba mnono mpya
lakini kaka na meneja wa mchezaji huyo – Rene Ramos ameshaifahamisha
Madrid lengo la mteja wake kutaka kuanza maisha mpya sehemu nyingine.
Rene ameripotiwa kusema kwamba Ramos anataka kuhamia Old Trafford
wakati huu wa dirisha la usajili na klabu pekee ambayo anataka Madrid
ifanye nayo makubaliano ni United.

Note: Only a member of this blog may post a comment.