BILA
shaka wiki iliyopita mlifurahia mada ya n‘makosa ya wanawake, wanaume
katika kuridhishana’ kwani nilipata ujumbe (SMS) kutoka kwa watu
mbalimbali wakielezea kuguswa na mada hiyo.
Wapo walioomba ushauri wa jinsi ya kumtendea mume ili ndoa iwe na
Amani muda wote. Lakini kuna ujumbe wa mwanamke mmoja ulinifikia
akilalamikia kuhusu tabia iliyokomaa ya mumewe kulala na suruali mpaka
asubuhi. Na mimi nikaamua kutumia malalamiko hayo kuwa ndiyo mada ya
wiki hii.
Kwanza mwanamke mwenzangu unakubali vipi mumeo alale na suruali
halafu unamlalamikia mtu mwingine wakati chanzo ni wewe? Kwani mafunzo
uliyopewa kwenye kitchen party hukuyafanyia kazi? Unamuaibishaje somo
wako na hata wazazi walioungana kuhakikisha unafundwa mpaka unakwenda
kuolewa.
EPUKA HILI
Leo nakukumbusha wewe mwanamke mwenzangu kwamba, mume hata kama
atarudi nyumbani amelewa chakari na ni usiku wa manane usithubutu
kumuacha akalala na suruali au na nguo alizorudi nazo. Hii ni aibu yako
mwanamke.
Kwanza kabla sijakwambia nini cha kufanya, nakusihi usije
kueleza siri hiyo kwa shoga yako kwamba mumeo analala na suruali,
walahi yeye ndiye atakuonesha jinsi ya kumvua nguo mumeo kwa sababu wewe
umeshindwa na umebaki kulalamika tu.
KUMBUKA
Mume anaporudi nyumbani mke unatakiwa kumpa mapokezi yasiyo na mfano.
Hii inahusu mume anapotoka kazini au kwenye mihangaiko yake mingine
bila kujali amerudi na nini au alikwenda kufanya nini.
FUATA MFUMO HUU
Mume akishaingia ndani tu, kabla hujafanya chochote, mpe pole kwa
kazi kisha mpeleke chumbani ukamvue nguo wakati umeshamwandalia maji ya
kuoga na nguo zinazotakiwa kwa ajili ya faragha.
Kwanza unapomuacha mumeo alale na suruali mtakulaje msosi wa usiku?
Kwa maandalizi hayo si rahisi mwanaume kulala na nguo mpaka asubuhi kwani atajua lazima mke utamuuliza kuna nini!
Nikwambie wewe ambaye mumeo anakufanyia hivyo maandalizi yako ni
hafifu ndiyo maana unalalamika na kutaka msaada kutoka kwa watu wengine.
EPUSHA UGOMVI ILI NDOA YAKO IWE NA AMANI
Ugomvi katika ndoa ni sumu kubwa sana, jichunguze ni kwa nini mumeo
analala na suruali, huenda mna ugomvi ambao ili kuwa na Amani na
kumfanya mumeo afurahie huduma zako jitahidi kutokuwa na ugomvi na kama
una kitu moyoni kiweke wazi hali hiyo itakufanya kuwa na uhuru na mumeo
naye kuwa karibu na wewe.
AIBU KWA MUMEO NI SUMU
Wanawake Wengi wana aibu kuwaonesha waume zao mahaba hasa hayo ya
kutaka kumchojoa, utaachwa na wale wasiokuwa na aibu watamchukua mumeo
hivihivi unaona.
Kuna wanawake mitaani nyuso zao hazina haya wala soni achilia mbali
aibu, ohoo! Kumbuka kuwa huyo ni mumeo, ni sawa na mwili wako tu
jitahidi uwe naye huru.
NAFASI YA MKE
Mwanamke mwenzangu, wewe ndiyo mkuu wa serikali yako hapo nyumbani,
kwa hiyo linapokuja suala la malezi kumbuka wewe ndiyo unamlea baba na
watoto.
Sasa iweje mumeo akushinde wakati kakuteua yeye mwenyewe?
Jitume ipasavyo kwenye kila idara uone kama mumeo atapindua, wengi
mnaharibu ndoa zenu kwa sababu ya kushindwa kutambua ujanja kama huu au
kuzembea kuyafanyia kazi mliyofundishwa na wafundaji wenu.
Naamini Wanawake wote mmenielewa kwani nimeongea lugha inayoeleweka Afrika Mashariki.
Tukutane tena wiki ijayo, bai!
Thursday, June 18, 2015
ACHA USHAMBA! KWA NINI UNAMUACHA MUMEO ANALALA NA SURUALI?
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
MAPENZI
on Thursday, June 18, 2015

Note: Only a member of this blog may post a comment.