Mwandishi wetu
Mtoto wa kike wa staa wa sinema
za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson aliyejifungua mwishoni mwa wiki
iliyopita na kumpa jina la Cookie (keki ndogo lakini tamu) anaanza
kung’aa kwenye vyombo vya habari baada ya baadhi ya watu kumpiga zengwe
la madai kwamba eti hafanani na baba yake, Moses Iyobo ‘Moze’.
“Unajua tangu akiwa mjamzito kuna watu walikuwa na shauku ya kumuona mtoto kujua kama kweli ni wa Moze maana mwanzoni hakuna aliyeamini kama mimba ni ya Moze ‘so’ hao ndiyo wameanza chokochoko,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutochorwa gazetini.
Aunt Ezekiel Grayson akiwa na mwanaye.
Baada ya kunasa zengwe hilo, Amani lilimtafuta Aunt ili azungumzie ishu hiyo ambapo alifunguka;Amani: Kuna zengwe juu ya baba wa mtoto wako, kwani mwanao anaitwa nani?
Aunt: Anaitwa Cookie Lapri-Center.
Amani: Yaani Lapri-Center ndiyo jina la ukoo?
Aunt: Mambo mengine hayawahusu. Mnataka jina la ukoo la nini?
Amani: Watu wanauliza, wanataka kujua maana tayari kuna zengwe juu ya baba wa mtoto.
Aunt: Acheni mambo yenu (kisha akakata simu).
Aidha, madai kutoka kwa chanzo chetu ni kwamba baada ya kuibuka kwa zengwe hilo, Aunt ameamua kumficha mtoto wake.
1 comments:
Write commentsKitanda hakizai halamu bana nyie vp,!
ReplyNote: Only a member of this blog may post a comment.