Sio tukio la kawaida kukutana na mtu
kavaa gauni la harusi kwenye mazishi.. kwenye headlines za 254 jirani
zetu wa nguvu Kenya kuna hii stori kutoka Kaunti ya Vihiga, unaambiwa
mwanamke aliyefiwa na mume wake akalazimishwa kuvaa gauni ambalo anavaa
bibi harusi wakati wa kufunga ndoa, alafu safari ya kwenda kwenye
mazishi ikaanza.
Mary Akatsa ni kiongozi wa Kanisa la Jerusalem Church of Christ
alikuwa akiongoza kila kitu mpaka mazishi yalipoisha, ukicheki kwenye
hii video huyo mama anaonekana mkali hivi kama unaenda tofauti na
maagizo yake.. wengine wanapigwa mpaka vibao.
Mazishi yalikuwa kama sherehe tu, kama
ukiiona hii video unaweza kuhisi labda watu walikuwa kwenye harusi au
sherehe nyingine ya kawaida.
Unaambiwa huu ni utaratibu wa kawaida
kabisa kwa waumini wote wa kanisa hilo, ikitokea mwanamke kafiwa na mume
wake lazima avae shela la harusi siku ya mazishi ya mume wake.
Bonyeza play au download video hiyo hapa chini....
Bonyeza play au download video hiyo hapa chini....
Note: Only a member of this blog may post a comment.