Tuesday, May 26, 2015

Anonymous

Nampenda sana WEMA SEPETU ila bado ana chuki na mimi – KAJALA

Kajala Masanja amesema hadhani kama ni rahisi kuwa karibu tena na Wema Sepetu baada ya kugombana.
Kajala amekiambia kipindi cha The Sporah Show hivi karibuni kuwa bado anampenda Wema na kumheshimu.

“Mimi simchukii Wema, mimi nampenda Wema, kusema ningependa kurudisha urafiki na Wema inakuwa ngumu sana, kwa sababu yeye tayari anachuki na sijui ana chuki kiasi gani? Mimi nataka kusema ni mtu ambaye nampenda na nakaaga nasema namheshimu, ni mtu ambaye alinisaidia,” alisema Kajala.

Pia Kajala amekanusha kutembea na mpenzi wa zamani wa rafiki yake huyo hali iliyozua ugomvi baina yao na kusababisha mpaka sasa kutoelewana.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.