Siku tatu baada ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (TABOA), kuendelea na msimamo wa kugoma nchi nzima kupinga nauli mpya, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imenywea na kufuta agizo lake la awali la kupunguza nauli hizo.
Badala yake, Sumatra imetangaza
kusitishwa utekelezaji wa viwango vipya vya nauli vilivyotangazwa hivi
karibuni na kutaka vya zamani viendelee.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sumatra kwa vyombo vya habari, jana jijini Dar es Salaam, na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu, Gilliard Ngewe, utekelezaji utasitishwa hadi marejeo yatakapofanyika tena.
“Sumatra
imepokea kutoka kwa msafirishaji ABC Trans na Afritrans Limited maombi
ya kupitia upya maamuzi yake ya kushusha viwango vya nauli za mabasi ya
masafa marefu yalitolewa Aprili 15, mwaka huu. Maombi ya Kampuni mbili
yalipokelewa Sumatra Aprili 29, mwaka huu, ,” alisema.
Alisema kwa sasa viwango vya nauli vya zamani vitaendelea kutumika hadi hapo umma utakapotaarifiwa vinginevyo.
Afisa Uhusiano wa Sumatra, David Mziray,
alisema sheria inatoa haki kwa wahusika kukata rufaa ndani ya siku 14
na kwamba kwa sasa wanapitia hoja zao kuona kama zina mashiko ndipo
watatoa maamuzi ambayo yatawekwa wazi.
Alisema viwango vipya vya nauli
vilitolewa baada ya kukokotoa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na kwamba
mambo yatawekwa wazi ndani ya siku 14.
Note: Only a member of this blog may post a comment.