Wilbert Molandi,Dar es Salaam
Ni mwaka wa neema kwa kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Deus Kaseke kwani ameitwa Taifa Stars siku chache baada ya kujiunga na klabu hiyo ambayo ni bingwa wa Tanzania Bara.
Kaseke, sambamba na Gadiel Michael wa Azam FC, kipa Said Mohammed na Andrew Vincent wa Mtibwa Sugar, wameongezwa katika kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mechi za kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) na Michuano ya Wachezaji wa Ndani (Chan).
Championi Jumamosi lilimshuhudia Kaseke katika mazoezi ya Taifa Stars jana asubuhi kwenye Uwanja wa Karume akiwa sambamba na wenzake walioitwa.Kaseke alisema: “Jana (juzi) ndipo nilipoitwa Taifa Stars, hivyo nikaja kwa ndege jioni yake na leo (jana) ndiyo unaniona hapa mazoezini. Nimejiandaa kupambana ili kupata nafasi kikosi cha kwanza.”
Awali, Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij, aliwaita wachezaji 16 kuwaunganisha na wale walioshiriki michuano ya Kombe la Cosafa huko Afrika Kusini ambapo watachujwa na kubaki watakaocheza dhidi ya Misri mwezi ujao kufuzu Afcon 2017.

Note: Only a member of this blog may post a comment.