Tuesday, May 26, 2015

Anonymous

KWISHNEI! Huu ndio uamuzi wa Real Madrid kuhusu hatma ya Kocha Ancelotti baada ya Klabu kuwa na matokeo mabaya!!

Siku mbili baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Hispania huku mabingwa waliopita wa Ligi ya mabingwa wa Ulaya, klabu ya Real Madrid kumaliza msimu bila kikombe chochote, leo hii klabu hiyo imetoa uamuzi kuhusu hatma ya kocha wao Carlo Ancelotti.
Kikao kimefanyika muda mfupi uliopita huko Madrid, Spain.. Rais wa klabu hiyo Florentino Perez ametangaza rasmi kwamba klabu hiyo imemsitishia ajira kocha huyo raia wa Kiitaliano.
Ancelotti alijiunga na Real Madrid miaka miwili iliyopita na kufanikiwa kuipa klabu hiyo ubingwa wa Ulaya, kombe la Copa Del Rey na UEFA Super Cup.
Makocha Rafael Benitez na Jurgen Klopp sasa ndio wanapewa nafasi kubwa ya kuirithi nafasi ya Ancelotti Santiago Bernabeu.
Sehemu ya rekodi ya Ancelotti wakati akiwa na Klabu ya Real Madrid. Cristiano Ronaldo huenda akawa mmoja ya mastaa wa Madrid walioumizwa sana na uamuzi huu kutokana na imani aliyokuwa nayo kwamba bado wataendelea kuwa pamoja na Kocha huyo japo mambo hayakuwa sawa msimu huu.
Real Madrid's Cristiano Ronaldo from Portugal gestures during a Spanish La Liga soccer match against Malaga at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid, Spain, Sunday, March 18, 2012. (AP Photo/Andres Kudacki)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.