Thursday, May 28, 2015

Anonymous

Mtoto wa Frolah Mvungi na H. Baba aitwaye Tanzanite acheza filamu kama ‘Albino'

Flora Mvungi na Mtoto wake Tanzanite
Mtoto wa msanii wa Bongo Fleva,H: Baba na mwigizaji wa Bongo Movie,Frolah Mvungi,Tanzanite amecheza filamu kama mhusika mkuu.

Akizungumza na Clouds FM, H:Baba alisema kuwa katika filamu hiyo ambayo hajaitaja jina Tanzanite amecheza kama mtoto aliyetekwa na watu waliodhania kuwa mtoto huyo ni mlemavu wa ngozi ‘Albino’.

‘’Mimi na Frolah tumecheza kwenye filamu hiyo na Tanzanite kama mtoto wetu amecheza nafasi nne kwenye filamu hiyo kuna watu wanamteka mtoto wangu wakidhani kuwa ni albino ndiyo maana tulimpaka hina kichwani ili afanane lakini baadaye wanagundua kuwa mtoto huyo siyo albino,’alisema H:Baba.
Hiyo ni filamu ya tatu wasanii hao kumshirikisha mtoto wao chini ya kampuni yao ya Double H Film

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.