Marehemu Rachel Haule
Na Hamida HassanMkurugenzi wa Kampuni ya Five Effects, William Mtitu hivi karibuni aliwalipua wasanii wenzake na kusema kuwa inavyoonekana kwa Mungu hawapo kwani wamekuwa wakichenga kwenda kanisani na msikitini inapotokea kuna kisomo kwa ajili ya marehemu.
Mtitu alizungumza hayo alipokuwa makaburini Kinondoni jijini Dar, kwenye misa ya mwaka mmoja ya marehemu Rachel Haule ambapo wasanii walifika makaburini kwa wingi lakini kanisani hawakwenda.
“Yaani watu wameibuka kaburini, kwa nini hawakwenda kanisani? Mastaa ni watu wa ajabu sana, inavyoonekana hawapo kabisa kwa Mungu, hili ni jambo la kusikitisha kabisa na kwa kweli tunatakiwa kubadilika,” alisema Mtitu.


Note: Only a member of this blog may post a comment.