Gavana wa jimbo la Edo la nchini Nigeria, Adams Oshiomhole,
amemuelezea mke wake, Iara, kama mlimbwendwe kwenye moyo wake na kwamba
si kwamba hajamuoa kuziba pengo la mke wake aliyefariki.
Akiongea kwenye misa ya shukrani kwenye kanisa la Immaculate
Conception Cathedral, Auchi, Jumapili iliyopita, Oshiomhole alizipuuzia
ripoti kuwa mke wake ni model maarufu na kudai kuwa maneno hayo
yametokana na urembo wa mke wake.
“Ninaposoma habari za kwenye magazeti na wanasema kuwa Comrade ameoa ‘mlimbwende’ mimi nasema labda ni mtu mwingine,” alisema.
“Msichana ambaye Mungu amleta kwangu kumuoa hakuwahi na si
mlimbwende. Of course, ni mrembo na naelewa kwanini watu wanadhani
msichana wa aina hii anaweza kuwa model, of course, ni model moyoni
mwangu na tuna tumaini na kuomba kwenye moyo wa Mungu wetu na nadhani
hicho ndio kitu muhimu.”
Gavana huyo ana umri wa miaka 63 huku mke wake huyo mpya ana miaka
36. Mrembo huyo ni raia wa Cape Verde na alifunga naye ndoa weekend
iliyopita.
Ndoa yao ilifungwa mbele ya wageni akiwemo rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na mtu tajiri zaidi Afrika, Aliko Dangote.
Ndoa hiyo imekuwa gumzo kwenye bara zima la Afrika.
-via bongo5
-via bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.