Nick Jonas na Kendall Jenner.
New York, Marekani
NICK Jonas na Kendall Jenner awali baada wa kuripotiwa
kuwa wanatoka kimapenzi, iliaminika kuwa ingekuwa bonge la kapo, lakini
ghafla msanii wa muziki na muigizaji huyo, kachomoa kuwa wala hatoki na
mwanadada huyo.
Nick Jonas .
Kendall ambaye ni mdogo wa mtangazaji wa Kipindi cha Keeping Up With
The Kardashians, Kim Kardashian, amewahi pia kuripotiwa kutoka na mkali
wa Langalanga, Lewis Hamilton.
Nick ambaye ana vipaji vingi vikiwemo kuigiza, kuimba na mwandishi wa
nyimbo, mapema wikiendi iliyopita, aliibuka na kusema kuwa Kendall ni
msichana mrembo sana lakini hawatoki kimapenzi japokuwa wamekuwa
wakionekana pamoja.
Nick aliyazungumza hayo wakati akiwa kwenye mahojiano na kipini cha
TV mwishoni mwa wiki iliyopita na kusema kuwa akili yake kwa sasa ipo
kwenye kazi zake za muziki.”Ni msichana mzuri lakini hatupo kimapenzi,”
alisema Nick wakati akiipromoti singo yake ya ‘Levels.’

Note: Only a member of this blog may post a comment.