Monday, May 18, 2015

Anonymous

HUU NDIO UKWELI KUHUSU DIAMOND PLATNUMZ NA ALLY KIBA KUCHONGANISHWA!

Kwa sasa kuna kampeni inaonekana kuundwa kwa lengo la kumshusha kisanii Diamond Platnumz na kumpaisha eti Alli Kiba !
Kwa asilimia kubwa Wanaoua sanaa ya Tanzania ni wasanii wenyewe, media na mashabiki halafu baadaye wanaanza kutafuta mchawi kumbe wanajiroga wenyewe.

Hiki tunachokifanya sasa kutaka kumshusha kinguvu Diamond na kumpaisha Kiba kisanaa bado tu hatujajifunza kupitia kifo cha Steven Kanumba?.

Kanumba alipokuwa hai alipikiwa majungu ya kila aina na wasanii wenzake kisa tu alikuwa juu, media hasa magazeti ya udaku hayakumuacha hivi hivi, magazeti ya udaku bila aibu yalidiriki kumuita Kanumba bogus eti hajui kiiingereza kisa aliingia jumba la Big Brother 2008.

Ila baada ya Kanumba kufariki sote tunajua jinsi kifo chake kilivyoathiri tasnia ya filamu nchini.

Bila aibu wale wasanii wenzake, media na mashabiki waliokuwa wakimponda Kanumba wakaanza kumsifia kinafiki eti alikuwa gwiji la sanaa na kifo chake kimeathiri sanaa ya filamu.

Mara baada ya nominations za kili Awards 2015 kutoka baadhi ya watangazaji wa Radio wakawa wanatangaza radioni Ali Kiba ndio anaongoza kwa nominations wakati ukweli sio kiba ana nominations 7 na diamond nominations 10.

Baadhi ya wasanii baada ya kuona Wema Sepetu na Ivan Ssemwanga(ex husband wa Zari) wanamsuppport Kiba lakini kukionekana kuna kitu kimejificha ndani yao hasa kumkomoa Zari na Diamond nao wakaanza kumpigia promo kiba.

Ndio ni kumkomoa Diamond kwasababu kama Wema bado angekuwa na Diamond asingethubutu kumfanyia kampeni kiba ingawa ni uhuru wake lakini bado hauna nguvu kwani hakuwahi kufanya hilo kipindi cha nyuma na pia hivi karibuni iliripotiwa kuwa Wema alizuiliwa kuingia kwenye show ya kiba huko Moshi/Arusha.

Hivi tujiulize hakuna wasanii wengine wazuri wa kuwapigia kampeni na kuwapaisha kama kina Rich Mavoko, Barnaba, Dimpoz, Mo Music na wengineo ila kiba ndio msanii pekee wa kupigiwa kampeni dhidi ya Diamond?.

Ukweli ni kuwa Diamond mwaka jana amefanya kazi kubwa kuliko Kiba ila unafiki na ushabiki ndio umewajaa baadhi ya watu.

Ni wazi kuwa tayari Diamond ana mchango mkubwa katika music wa Bongofleva ndani nje ya nchi kuliko Kiba ambaye amemtangulia lakini alishindwa kutumia fursa kipindi hicho ila kwasasa anataka kutumia jina la Diamond Platnumz kurudi kileleni, if not kwanini kiba asipambanishwe na wasanii wengine wakali kama Rich Mavoko?.

Kiba anabebwa sana kwa promo unfortunetly juhudi zake za kufika mbali kisanaa kama alipofikia Diamond bado ni changamoto kubwa kwake sababu amebebeshwa mzigo mzito chini ya uwezo wake.

I like Kiba lakini tuseme kweli kuwa hili linaloendelea sio zuri kwa mustakabali wa music wetu wa Bongofleva, nathubutu kusema hizi ni hila dhidi ya Diamond kwasababu tayari ilishajirudia zaidi ya mara 2 Diamond kufanyiwa hujuma katika majukwaa ya show anapokuwa ana-perform na kiba hurushiwa chupa, huzomewa bila sababu lakini hujuma hizo hazitokei Diamond anapofanya show jukwaa moja na wasanii wengine au peke yake.

Anyhow, mfano Kiba akipata tuzo 5 au zote 7 Kili Awards mwaka huu basi ni matumaini yetu pia aanze kupasua kimataifa kama alivyofanya Diamond kwa kuitumia fursa iyo na sio kubaki tena kuishia hapa Tz.

Mfano Diamond akishuka kisanaa au kupata tatizo(Mungu aepushie mbali) ndio mchango wake utajulikana na wakati huo kukiwa hakuna wa kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania kimataifa kama yeye.

Hata kama hahusiki moja kwa moja na suala hili Ali Kiba angekuwa mstaarabu na kama mtu aliyemtangulia kisanaa Diamond asingekubali hili litokee majukwaani akishuhudia badala yake angekuwa karibu na Diamond na kufanya kazi pamoja, lakini matokeo yake suala hili linamshusha pia Ali kiba kwa watu au mashabiki ambao walimuona mtu wa maana sana hapo awali.

Tusim-judge Diamond kwa maisha yake binafsi lets judge his music, Kiba ameficha sana maisha yake personal ndio maana wengi wanamuona mtakatifu.

Wabongo walimponda sana Diamond lakini alipoanza kuthaminiwa nchi za nje na sisi kwa kuona aibu tukaanza kumthamini.

Kama ni promo basi kiba apewe promo ya kawaida kama wasanii wengine lakini sio promo za aina hii kwa lengo la kukomoana na mwisho wa siku kushusha muziki wetu na sio kuukuza MWISHO:

Sina tatizo na Kiba na wala simjui Diamond personally zaidi ya kumuona kwenye media na events.
I once met Diamond at UDOM in 2010 and we had a photo together but mpaka leo sijawahi kumpa salamu ya face to face.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

1 comments:

Write comments
Unknown
AUTHOR
May 19, 2015 at 5:31 AM delete

Mti wenye Matunda ndo hupigwa mawe,.! so DIAMOND hashikiki jaman" kwanza anaiwakilisha Tz vzur nje,! kwann asipewe pongez yake..! Afu mselang KIBA" mbona hufanani na huo upuuzi unaoendelea kama huwapi sapoti kwa ujinga huu mashabiki wako kwanin usiwakemee? Tunataka kila kizur kiletacho mafanikio ktk nchi yetu kipewe sapoti sio kuleteana majungu kushushana mwishowe Tz yetu Iwe na sifa mbovu...! Elimu mbovu" Siasa mbovu" Uchumi mbovu" Sanaa mbovu" Maisha mabovu"..! Why KIBA sio ishu Man ..! Tunazikubali kazi zako ila sio majungu na fitina zako..! AMBIA KIBA TIM SIO ISHU Bazeee,,,,,,,!

Reply
avatar

Note: Only a member of this blog may post a comment.