Thursday, May 14, 2015

Anonymous

ACT yaomba kujiunga UKAWA

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe katika moja ya mikutano ya chama hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mgwira amesema chama hicho hakina matatizo na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na hata sasa kinasubiri majibu ya barua yao waliyoituma kwa umoja huo kuomba kuunganishwa. 

Mgwira alitoa kauli hiyo wakati chama hicho kilipofanya ziara ya kutembelea hospitali ya mkoa ya Mt Meru kugawa zawadi mbalimbali katika wodi ya kinamama ikiwa ni njia ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake. 

Alisema ACT-Wazalendo wanaunga mkono muungano wowote wa vyama vya upinzani nchini ulio halali.

“Hatuna matatizo na Ukawa tunaunga mkono muungano wowote wa upinzani ulio halali,” alisema kiongozi huyo 

Alisema tangu waandike barua ya kuomba mwongozo wa namna ya kujiunga na Ukawa, bado hawajapata mrejesho.

“Tunatamani kuunganisha nguvu katika siasa za vyama vya upinzani na sasa tunasubiri majibu ya barua yetu ya kuomba kuingia Ukawa,” . 

Alisema kuwa chama hicho kimepokewa vizuri na wananchi wa mikoa mbalimbali nchini na katika ziara ya awamu ya kwanza walifanikiwa kuingiza jumla ya wanachama wapya 700.

Tumepokewa vizuri mikoani tumefanikiwa kuingiza wanachama wapya na hoja ya umoja na uzalendo watu wameipokea vizuri,”  Mgwira. 

Akipokea misaada katika hospitali hiyo Muuguzi Mfawidhi, Sifael Masawe alisema kwamba misaada hiyo itasaidia kupunguza shida za wagonjwa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.