Awali ya yote naomba niseme kwamba, safu hii ni kwa ajili yako wewe
msomaji wangu. Huenda una jambo ambalo ungetamani nilijadili hapa au
labda una tatizo linalokukosesha amani katika maisha yako ya kimapenzi,
usisite kunitumia ujumbe kupitia namba zangu hapo juu nami nitakufanya
uwe na amani.
Mpenzi
msomaji wangu, nilishawahi kusema huko nyuma kwamba mapenzi yanachukua
sehemu kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku.Tunafanya kazi usiku na
mchana lakini pesa tunazopata tunazitumia kwenye kufurahia maisha na
wapenzi wetu.
Ndiyo maana ukiwa hauko sawa kimapenzi, namaanisha ukiwa huna mpenzi wakati unahitaji kuwa naye au unaye lakini anakukorofisha mara kwa mara, hata mambo mengine huwezi kuyafanya kwa ufasaha. Lakini yule ambaye maisha yake ya kimapenzi yako sawa, anapata anachokitaka kutoka kwa mpenzi wake, utagundua anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na furaha haikauki moyoni mwake.
Wakati ukweli ukiwa hivyo, wapo ambao wanaachika kila siku kwa sababu ya kushindwa kujua namna ya kuwashika wapenzi wao. Kuna ambao kusalitiwa kumekuwa ni sehemu ya maisha yao kwa sababu hawajui yapi wayafanye ili wapenzi wao wasifikirie kutoka nje ya uhusiano wao.
Kimsingi nimegundua wengi hatuna elimu ya kutosha juu ya mapenzi. Unakuta mtu kaanzisha uhusiano na mtu ambaye yuko mbali lakini au wote ni wafanyakazi, hawajui wanawezaje kulidumisha penzi lao.
Hayo yote utayaelewa endapo tu utajua sehemu sahihi ya kuweza kujifunza na kuwa na ufahamu kuhusu mambo hayo.
Huenda wewe tangu umezaliwa hujawahi kujihusisha kimapenzi, leo umeingia kwenye uhusiano na hujui chochote, kama huna elimu ya mapenzi hata kama umzuri vipi, utaachika tu kama siyo kusalitiwa kila siku.Ndiyo maana leo nimeleta mada hii ili kama ulikuwa hujui, uanze leo kujiimarisha kwenye masuala ya mahaba. Hata hivyo, mbinu za kujifunza elimu ya mapenzi zipo nyingi lakini leo nikupe tatu tu ambazo ni rahisi kwako kuzitumia.
Kwanza ni kupitia mitandao mbalimbali inayozungumzia masuala ya mapenzi.
Mitandao imekuwa ni msaada sana katika ulimwengu wa sasa. Hakuna ambalo utalihitaji usilipate kwenye mtandao. Kwa maana hiyo basi, kama kuna jambo unataka kulijua kuhusu mapenzi, kuwa rafiki wa mitandao husika.
Kwa mfano unataka kujua jinsi unavyoweza kumfurahisha mpenzi wako mkiwa faragha. Ukiuliza mtandao, utakuletea.
Licha ya kwamba lugha inayotumika ni ya Kiingereza, naamini wengi wetu tunajua hata kama ni cha kubangaiza. Ila zipo baadhi ya mada ukiandika kwa Kiswahili pia unaweza kuzipata.
Pili, hakikisha unanunua majarida mbalimbali ambayo ndani yake kuna masuala ya mapenzi. Majarida hayo yapo kila kona. Kama kweli wewe ni mtu mwenye uhitaji wa majarida hayo, ukiulizia utayapata kwani huwezi kuyakuta yanauzwa kiholela.
Wakati mwingine yanauzwa bei kubwa lakini elimu utakayoipata ni kubwa na huwezi hata kujutia fedha uliyotoa. Kwa mfano unanunua jarida la shilingi 20,000 na ndani yake ukapata mada juu ya kuishi kwa furaha na mpenzi wako, namna ya kuidumisha ndoa yako, jinsi ya kumpagawisha mpenzi wako muwapo faragha na kadhalika. Huoni itakuwa ni pesa ndogo ukilinganisha na faida utakayoipata?
Tatu, watafute wataalam wa masuala ya mapenzi na hata ukitakiwa kuwalipa usione ni hasara. Kuna wataalam ambao wanaweza kukusaidia kuwa bora katika ulimwengu wa mapenzi. Kwa mfano mimi nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi kushauri wasomaji wangu kuhusu mambo yanayowakosesha furaha katika maisha yao ya kimapenzi.
Siyo mimi tu, wapo wengi wakiwemo baadhi ya akinamama ambao wamekuwa wakitumika sana kwenye kuwafunda wasichana kabla ya kuingia kwenye ndoa.Kikubwa ni kujua watu sahihi wa kuwauliza mambo sahihi kuhusiana na mapenzi.
Nilichogundua ni baadhi ya watu kuwa na aibu. Hivi unaonaje aibu huku unataka kujua mambo nyeti ambayo unajua kutokuyafahamu kunaweza kuihatarisha ndoa yako?Ndugu yangu, mapenzi si jambo la kulichukulia kimzaha. Wapo ambao najua hawana amani kwa sababu wapenzi wao wanaeleza wazi kutokipata kile walichokitarajia.
Hakika changamoto ni nyingi sana kwenye suala la mapenzi lakini nakuomba fanya kila unaloweza kuhakikisha unakuwa bora katika eneo hilo. Usiona aibu kujifunza, aibu yako itakufanya uendelee kuwa mbumbumbu na hakika hutaweza kuyafurahia maisha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.