Hans Mloli,Dar es Salaam
YANGA noma sana! Ikiwa imebaki takriban wiki moja kabla ya kuvaana na wapinzani wao Etoile du Sahel ya Tunisia, tayari timu hiyo imejizatiti na kuwafanyia ushushushu wa hali ya juu Waarabu hao kiasi cha kubaini mbinu zao zote tangu walipoanza maandalizi ya awali ya kuvaana nao na sasa ina kila kitu mkononi.
Timu hizo zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wao wa kwanza wa raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho wiki ijayo Aprili 18, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kabla ya kurudiana nchini Tunisia wiki mbili baadaye.
Lakini Yanga kwa kutambua fitna za Waarabu, mapema ikaamua kujizatiti na kuanza kuifuatilia timu hiyo kwa kumtumia mtu wa ndani wa timu hiyo kwa ajili ya kuchimba kila kinachoendelea na kukivujisha kwa Yanga.
Imeelezwa kuwa shushushu huyo ambaye hakuwekwa wazi asili ya nchi yake ni wapi, ana urafiki kama si ujamaa mkubwa na Kocha Mkuu wa Yanga, Mdachi, Hans van Der Pluijm, hivyo kila kitu kinafika kwa wakati muafaka na Yanga nayo ikiendelea kufanyia kazi kila inachokipata.
Mmoja wa viongozi wakubwa wa Yanga ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, amelitonya Championi Jumatatu kuhusiana na mipango hiyo ambapo alikiri kuzijua fitna za Waarabu hao, hivyo na wao safari hii wameamua kuingia vitani kuhakikisha wanafanikiwa kuvuka hapo walipo sasa na kusonga mbele.
“Kila mmoja anafahamu fitna za Waarabu na uwezo wao wa kisoka, hivyo ni lazima na sisi tujipange.
“Tayari tuna mtu wetu yupo kule, anawasiliana na sisi bila tatizo, tena mipango mingi zaidi inaifikia benchi la ufundi, maana wao ndiyo wana dhamana kubwa kuhusu timu, jamaa ni mtu wa Etoile, yupo ndani ya Etoile na ni rafiki mkubwa sana wa Pluijm, kwa hiyo imekuwa vizuri zaidi katika hilo, maana kila kitu kinatufikia na tunajua kinachoendelea.”
Hata hivyo, gazeti hili lilipozungumza na Pluijm kuhusiana na maandalizi kwa ujumla kuelekea katika mchezo huo, alizungumza kwa kifupi huku akisisitiza kuwa muda muafaka wa kuweka hadharani mbinu zao bado haujafika.
“Naifahamu Etoile, ni timu nzuri lakini siwezi kuwazungumzia sana kwa sasa kwa sababu bado tunaendelea kujipanga dhidi yao huku tukiwa na michezo mingine migumu ya ligi kama unavyojua lengo letu pia ni ubingwa wa ligi.
“Baada ya kumaliza mechi yetu na Mbeya City Jumapili hii (jana) nitajikita kwa asilimia zote sasa kwa ajili ya Etoile ila naweza kusema kwamba kila kitu kinakwenda sawa na hatutakiwi kuwa na hofu kwa kuwa tunayoyapanga yanakwenda kama yalivyo, isipokuwa tunahitaji morali na mbinu chache kwa ajili ya kuhakikisha tunaanza kwa ushindi katika mchezo wetu wa nyumbani,” alisema Pluijm.

Note: Only a member of this blog may post a comment.