Monday, April 13, 2015

Anonymous

SIMBA: HAINA KUREMBA!

Na Martha Mboma, Dar es Salaam
SIMBA imesema haitaki masihara tena katika mechi zake tano zilizobaki na imetamka hadharani kwamba inakwenda kuiangamiza Mbeya City katika mchezo unaofuata Aprili 18 kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
 

Simba kwa sasa imeshacheza michezo  21 na ina pointi 35 na tayari awali ilishavaana na Mbeya City katika Uwanja wa Taifa na kupoteza mchezo kwa mabao 2-1. Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkurugenzi wa Kitendo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Haji Manara, alisema kuwa lengo lao ni kuondoka na ushindi Sokoine. 

Manara alisema ili kuhakikisha wanafanya vyema, kikosi chao kitaanza kujiwinda mapema leo Jumatatu kabla ya kutimkia mkoani Mbeya.“Simba imebakiza mechi moja mkoani ambayo  itacheza dhidi ya Mbeya City na sisi tunahitaji alama tatu katika mchezo huo na Kopunovic ameahidi kufanya maandalizi ya nguvu kwa vijana ilikuweza kuonyesha kuwa mchezo wa kwanza tuliteleza  tu.
“Kwa ujumla sisi kama klabu na mipango ya mwalimu ni  kufanya vyema  na kuibuka na ushindi, bila kujali awali tulipoteza,  safari hii tunakuja kivingine kabisa kuweza kupambana,” alisema  Manara.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.