Wednesday, April 15, 2015

Anonymous

YALIYOTUFIKIA KUHUSU MWENYEKITI WA ACT WAZALENDO HAYA HAPA...

Wapo wale wanaodai kuwa pengine mama huyu amewekwa kwenye chama kuwa kiongozi kivuli, lakini pia wapo baadhi wanaobeza na kusema kuwa hataweza kuvaa viatu vya wanaume.
Huyo si mwingine, ni mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Anna Elisha Mghwira (56), mama wa watoto watatu, msomi mwenye taaluma ya sheria na tauhidi ( theolojia) na mzaliwa wa Singida . 


Gazeti la Mwananchi lilimfikia mama huyo akiwa ofisini kwake, Kijitonyama, Dar es Salaam akiendelea na majukumu yake ya kawaida na kupata mambo kadhaa kuhusiana naye.
Mwandishi: Imekuwaje hadi ukateuliwa na kumudu kuwa kiongozi wa juu kabisa wa chama chako? 


Mghwira: Pamoja na kuwa nimekuwa kwa muda mrefu katika shughuli zangu mbalimbali, lakini naweza kusema harakati zangu hasa zilianzia kwenye theolojia, elimu niliyoipata kutoka Chuo kikuu cha Makumira, Arusha. Pale, nilisomea theolojia katika mrengo wa kimapinduzi.

Nikiwa kwenye kozi hiyo pia nilipata wasaa wa kusoma na kuzijua kwa undani dini zote, ukiwamo Uislamu na Ukristo na kwa kuwa niliamini ndiyo jamii yenyewe siku zote nilikuwa na bidii ya kujua misingi yake. Jambo hilo kwa kiasi kikubwa lilichangia kuniongoza hadi hapa nilipo. 

Mwandishi: Unajisikiaje kusimama meza moja na wenyeviti wenzio wa vyama kama vile, Rais Jakaya Kikwete (CCM), Prof Ibrahim Lipumba (CUF), Freeman Mbowe (Chadema), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Augustine Lyatonga Mrema (TLP)?
Mghwira: Ni kawaida, siwezi kusema najivunia hilo kwani naamini, tuna uwezo sawa na ndiyo maana tunaweza kusimama meza moja. Ikitokea nikakutana nao siku moja nitawaambia, ‘usawa wa kijinsia unawezekana, lakini siyo kuutengeneza’. 


Wao kama viongozi wa vyama wanatakiwa wawape nafasi wanawake ili waonyeshe uwezo wao. Kwani naamini wako wenye uwezo kuliko wanaume.
Mwandishi: Viongozi wengi wa upinzani unaowaona leo ni mazao ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vipi kwa upande wako?

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.