Wakizungumza katika eneo la tukio watu waliokutwa na adha hiyo wamesema hali hiyo inatokana na miundombinu mibovu ya barabara na madaraja na imewasababishia mateso makubwa kwani baadhi yao walikuwa wanafuata huduma muhimu wanakoenda.
Wameitaka serikali iangalie barabara hiyo inayounganisha mikoa ya Simiyu, Shinyanga pamoja na Arusha.
Baadhi ya wakazi wa vijiji vya jirani na eneo hilo wamesema mafuriko hayo yamesimamisha huduma zote za kijamii katika eneo hilo kwa kuwa daraja lililojaa maji ndiyo kiungo muhimu cha kufika eneo yenye huduma.
Wamesema kwamba serikali mara kadhaa imeahidi kuliboresha bila matumani huku ikijuwa dawa pekee ya sehemu hiyo ni kujenga daraja refu na mwenyekiti wa kitongoji cha maokoni mkuya nyinyi akidai hata wagonjwa wameshindwa kwenda hospitalini.
-via ITV

Note: Only a member of this blog may post a comment.