Thursday, April 30, 2015

Anonymous

VIDEO: DUNIA IMEKWISHA! Wafanyakazi wa Mochwari Waiba Nguo za Maiti!

candle-light
Hii imeripotiwa toka Embu, Kenya.. nilipoiona nikadhani inafanana na ile ya Kibaha Tanzania ambako wezi walivunja kaburi na kuiba mabegi ya nguo ambazo marehemu aliomba azikwe nazo.. baada ya kuifatilia nikakuta hii iko tofauti kidogo, japo zote zinahusu matukio wanayofanyiwa marehemu. 

Familia waligundua kuwa mwili wa marehemu ndugu yao umewekwa kwenye jeneza bila kuvalishwa nguo wala viatu ambavyo walipeleka mochwari, lakini wafanyakazi wa mochwari hawakumvalisha nguo hizo.

Nguo zenyewe tulikuwa tumeleta haziko kwa mwili.. mwili umewekwa mitumba, tshirt ya mtumba, suruali ya mtumba hata viatu haikuwa imewekwa” alisema mmoja wa ndugu wa marehemu. 

Baada ya ishu hiyo kuwa na mvutano ilibidi ndugu wanunue nguo nyingine za kumvalisha ndugu yao, lakini bado walibaki na maswali ambayo hayakuwa na majibu, nguo walizoleta mara ya kwanza ziko wapi ??
Nimekuwekea taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24… Kutazama video ya tukio hilo bonyeza play hapa chini…

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.