JESHI la Nigeria leo limewaokoa mateka wengine 160 waliokuwa
wanashikiliwa na wapiganaji wa Kiislam wa Boko Haram katika msitu wa
Sambisa ambapo kwa sasa wanahesabiwa kuhakikisha idadi yao.
Hii imetokea ikiwa ni oparesheni endelevu ya kulisambalatisha kundi
la Boko Haram nchini humo, baada ya Jeshi hilo kuivamia ngome ya Boko
Haram iliyopo katikati mwa msitu wa Sambisa ampapo juzi wanawake 93 na
wasichana 200 waliokolewa na Jeshi la Nigeria kutoka mikononi mwa
wapiganji wa Boko Haram
"Bado tunawahesabu kupata idadi sahihi, lakini tayari kuna wanawake
60 wa umri mbalimbali na watoto wapatao 100,” alisema Kanali Sani Usman
akizungumza na shirika la habari la AFP, akaongeza kwamba tayari
wamepelekwa katika eneo salama.
Hata hivyo, katika oparesheni ya kuwapata, mwanamke mmoja aliuawa na wanane miongoni mwa mateka walijeruhiwa.
Vilevile, Aprili 28, jeshi la Nigeria liliwaokoa wanawake na wasichana 293 kutoka msitu huo.
NA MTANDAO WA PULSE

Note: Only a member of this blog may post a comment.