Martha Mboma, Bulawayo
KOCHA wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amefunguka kuwa si wakati wa kumtupia lawama kiungo wa timu hiyo, Said Juma Makapu kwa kuwa bado anahitaji muda kutokana na kutokuwa na uzoefu wa mashindano ya kimataifa.Makapu alidaiwa kucheza chini ya kiwango wakati Yanga ilipopokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa FC Platinum juzi Jumamosi.
Aidha, alisema kuwa kiungo huyo ni mzuri na kwa sasa bado anahitaji muda na siyo kukatishwa tamaa, alisisitiza Makapu ni kiungo mzuri na atakuja kuwa mchezaji tegemeo zaidi katika kikosi cha Yanga.
Alisema baada ya kuona upungufu wake ndiyo maana aliamua kumtoa na kumuingiza, Kelvin Yondani ambaye alibadili mchezo kwa kiasi fulani. Kocha huyo raia wa Uholanzi aliongeza kuwa katika kikosi chake hakuna mchezaji mwenye namba ya kudumu, hivyo ni lazima wachezaji wote watengenezwe.

Note: Only a member of this blog may post a comment.