
‘’ siri zimeanza kufichuka kwamba chama hicho kinamilikiwa “kinyemela” na kigogo wa juu wa chama cha Mapinduzi CCM’’.
Na KAROLI VINSENT
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata zinadai chama hicho kinafadhiliwa kwa ukaribu sana na Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta (pichani),kwa lengo kwamba endapo mambo yakienda hovyo ndani ya chama chake cha mapinduzi CCM kwenye wakati wa uteuzi wa mgombea wa Urais basi ajiwekee mazingira ya kukimbilia huko.
“Hapa sio Sitta tu wako wengi wameanza kujiweka mguu sawa kutafuta upenyo nje,na hapa watu wanasubilia tu maamuzi ya Kamati kuu ya CCM wakati wakupitisha majina tu upande wa urais na NEC iamue na hapa kuna kilauwezekano akapita mtu ambaye akipita tu chama kitakuwa na msuguano ndani kwa ndani “
“Na watanzania waviangalie vyama hivi vinavyoanzishwa kipindi cha Uchaguzi vingi vinakuwa ni vyama vya kimamluki tu vya watu wapenda madaraka tu,”amesema Kiongozi wa CCM kutoka mikoa ya Kaskazini.
Taarifa hizo zinakuja ikiwa teyari Mwenyekiti na Muasisi wa Chama hicho cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (CKUT), Ramadhani Semtawa kutangaza mara baada ya kupata usajili mda wakati wa mkutano na waandishi wa habari akisema wanamuomba Waziri Sitta kujiunga nacho kwani chama hicho wanadai kinaendana na Falsafa ya Ujamaa na kujitegemea iliyoasisiwa na Mwalimu Julias Nyerere.
Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wa Karibu wa Samwel Sitta aliyezungumza na Mtandao huu kwa sharti la kutotajwa jina anasema Waziri huyo anajihami ndani ya chama chake kutokana nguvu kubwa aliyonayo Kada mwenzake wa CCM,Edward lowassa ambaye anaonekana kupewa nafasi kubwa ya Urais hapo baadae kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kwa mujibu mtoa taarifa huyo anasema kitendo cha lowassa kuchukua nafasi ya Urais kutamweka sehemu mbaya Mbunge huyowa Urambo Mashariki ambapo amekuwa na mahusiano mabaya na Waziri Mkuu huyo wa zamani.
Duru zinasema Chama hicho cha (CKUT), kinachofuata itikadi iliyoijenga heshima Tanzania Miaka ya nyuma ya Ujamaa na Kujitegemea zinasema uwenda chama hicho kikiushangaza ulimwengu baada ya kutajwa kuwachukua Vigogo wengi wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao wanaojiona watakuwa na wakati mbaya akichukua nafasi Lowassa.
“Da mwaka huu mtashuhudia mengi sana,na watu wameshaona nguvu ya Pesa aliyokuwa nayo Lowasa ni kubwa sana,sio pesa teyari huyu bwana ameyateka makundi makubwa ndani ya nchi,yaani chama chake kishapata presha,na hii itakuwa sawa na Rais Kikwete ilivyokuwa mwaka 2005 naye alikuwa na magenge kama ya lowassa na alipingwa hivyo na kina mashishanga “.
“Na atapita tu huyu mtu,ndio maana wakina Sitta wanahaha sana na mwaka huu sijui ccm kama itabaki salama”imeelezwa.
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli na pia ni waziri mkuu aliyejiuzulu kwenye Kashfa ya Ufisadi wa Kampuni tata ya Richmound ambapo ni miongoni mwa makada wa CCM,wanaoutaka Urais kwa udi na Uvumba.
Ambapo inadaiwa anauhasama mkubwa na Samwel Sitta unatokana na maamuzi ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge Dk Heririson Mwakyembe yaliyomkaang’a mpaka akachukua uamzuzi kwa kujiuzulu ambapo mara kwa mara lowassa amekaliliwa na Vyombo vya Habari akisema ameonewa na Kamati hiyo kutoka na kutopatana na makada wenzake wa CCM.

Note: Only a member of this blog may post a comment.