Thursday, April 30, 2015

Anonymous

Riyama Ally: Najifunza kwa Thea!

Staa  wa Bongo Movies anayesifika kwa maadili na kuvaa uhusika kwenye kazi zake, Riyama Ally, ameibuka na kudai kwamba vitu vingi vya uigizaji hujifunza kutoka kwa msanii mwenzake, Ndumbaro Misayo ‘Thea’. 

Riyama alisema Thea ni msanii zaidi yake na huwa hajibweteki kwa kulewa sifa kama walivyo baadhi ya waigizaji, ndiyo maana hupenda kujifunza kwake.
“Mimi najiamini na huwa napenda kumpa pongezi mtu anayefanya vizuri katika sanaa, Thea tangu alivyoanza kuigiza hajawahi kutetereka kwa kuwa halewi sifa za mashabiki wake, hivyo ni mfano wa kuigwa na wasanii wengine,” alimaliza Riyama.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.