Thursday, April 30, 2015

Anonymous

PICHAZ: AJALI MBILI ZAUA NA KUJERUHI IRINGA!

Baadhi ya wananchi wa mjini Iringa na abiria wa basi la Embakasy wakitazama basi hilo lililopinduka leo eneo la Ipogolo mjini Iringa






AJALI yaua mmoja Iringa huku abiria 18 wakinusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Embakasy lenye namba za usajili T 997 AKJ kuacha njia ya kupinduka eneo la Ipogolo mjini Iringa.

Wakizungumza na mtandao huu eneo la ajali baadhi ya abiria wa basi hilo walidai kuwa basi hilo lilikuwa likitaka kuingia katika kituo kimoja wapo cha mafuta eneo hilo na wakati likitoka ndipo liliponusurika kugongana na lori lililokuwa barabara kuu ya Iringa - Mbeya .

Hivyo kutokana na kunusurika kugongana ndipo dereva wa basi hilo alipoamua kulikwepa lori hilo kwa kukata kona kubwa zaidi iliyopelekea basi hilo kuacha njia na kupinduka kando ya barabara hiyo .

Walisema kuwa basi hilo limekuwa likifanya safari zake kati ya Ilandutwa wilaya ya Iringa vijijini na Iringa mjini na kuwa pona yao katika ajali hiyo ni kutokana na kuwa katika mwendo wa kawaida zaidi .

Konda wa basi hilo Bw Esack Mtandi alielezea tukio hilo alisema kuwa basi hilo lilikuwa likitaka kuingia kujaza mafuta katika kituo kimoja wapo cha mafuta kilichopo eneo hilo na mbele kulikuwa na lori na wakati dereva akijiandaa kuingia kituoni hapo ghafla usukani uligoma na hivyo kumtoa dereva nje ya barabara kabla ya kupinduka.

Alisema katika basi hilo kati ya abiria 18 waliokuwepo abiria 6 ndio waliojeruhiwa akiwemo dereva na hakuna aliyepoteza maisha.

Kwa upande wake jeshi la polisi mkoani Iringa limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 3 kasoro asubuhi ya leo na kumtaja dereva wa basi hilo kuwa ni Abdalah Nyalusi.

Alisema kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi na kuwa katika ajali hiyo hakuna abiria aliyepoteza maisha .

Wakati huo huo mmoja kati ya wafanyabiashara maarufu mji wa Ilula wilayani Kilolo mkoani hapa aliyefahakika kwa jina moja la kasim aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 111 GRE RAV4 amekufa papo hapo baada ya kugongana uso kwa uso la lori.

Kamanda Mungi alisema kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akitokea Ilula kuja Iringa mjini na baada ta kufika eneo la kona ya Igumbilo barabara kuu ya Iringa - Dar es salaam wakati akijaribu kulipita daladala lililokuwa mbele yake katika kona hiyo ghafla alikutana na lori hilo na kugongana nalo .

Hata hivyo alisema jina kamili la mtu huyo bado kufahamika na kuwa wanasubiri ndugu zake ili kujakutambua mwili huo na kutoa jina kamili.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.