Monday, April 13, 2015

Anonymous

RAIS MSTAAFU OBASANJO AVUTIA WENGI KWA KUJIPIGA PICHA KWENYE SIMU YAKE

 
Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo akijipiga picha.
RAIS wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, amekuwa akiwavutia wananchi wenzake kwa kujipiga picha akitumia simu yake ambayo inatumia mfumo wa ‘android’.
Obasanjo amekuwa akimwagiwa sifa kibao kutokana na kwamba yeye ndiye aliyeruhusu kuingia kwa simu za mkononi wakati akiwa madarakani, jambo ambalo limerahisisha  shughuli za watu wengi nchini humo kutokana na teknolojia yake. 

Pamoja na kwamba umri wake ni mkubwa sasa, bado kiongozi huyo wa zamani ana muda wa kupumzika na kutaniana na marafiki zake wakati hana mzigo tena wa kuisimamia nchi yake mbali na kutoa ushauri tu anapotakiwa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.