Shetta amekiri kuwa ndoa yake ipo kwenye matatizo hali ambayo inaweza kuvunjika hatua stahili zisipochukuliwa.
Shetta ameiambia Bongo5 kuwa anaumizwa sana mambo yanayoendelea
kuzungumzwa bila ukweli wowote hasa kuhusu uhusiano wake na Rose Ndauka.
“Rose Ndauka ni mshkaji wangu, nilikwenda naye Morogoro kwenye msiba
na kukaa naye pamoja na kulala naye hoteli moja ndo limekuwa tatizo,”
amesema rapper huyo.
“Watu wanaoanisha sana na haya mambo wakati sio kitu cha ukweli.
Inasabisha mambo mengi kutokea kwa upande wangu. Kwa upande wa mke wangu
mambo siyo mazuri kidogo siyo sana, mambo siyo mazuri, vitu
vinavyoendelea kuzungumza ndo vinaongeza vitu vingine,” alisema Shetta.
-bongo5
-bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.