Monday, April 6, 2015

Anonymous

MASKINI SHAMSA FORD WA BONGO MUVI! NDOA YAKE KWISHNEI, MWENYEWE AANIKA MAZITO!

Imelda Mtema
Mshtuko! Weka pembeni mahaba niue waliyokuwa wakioneshana, staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka rasmi kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake ya kimila aliyofunga na mwanaume wake wa siku nyingi, Dickson ‘Dick’ akikiri kuwa amepoteza muda mwingi kwa mtu ambaye hakuwa na mapenzi ya dhati kwake.

Shamsa Ford akicheka baada ya kuulizwa swali alipotembelea Global TV Online.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shamsa alitiririka kwamba mara nyingi alikuwa akichezea kichapo tena akiwa na ujauzito wa miezi minne wa mtoto wao, Terry lakini kipindi chote hicho alikuwa akivumilia ili kukwepa aibu na kumlindia heshima.
Shamsa Ford akiwa na mumewe wake, Dickson Matoke.
“Dick ameninyanyasa kwa muda mrefu  lakini kuepuka aibu ya kuwa mastaa hawatulii, nikawa navumilia kipigo kikali hivyo niliamua kuachana naye tangu Oktoba, mwaka jana na sikutaka kusema ila sasa nimeweka wazi kutokana na yeye kuanika mambo yetu kwenye mtandao wa kijamii,” alisema Shamsa. Alipotafutwa Dick, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.