Watu wanane wakiwemo wanafunzi sita wa shule ya msingi Kibirizi,
mwalimu mmoja pamoja mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapo walipoteza
maisha hapo jana baada ya kupigwa na radi huku wanafunzi wengine 15
wakijeruhiwa na radi hiyo.
Miili ya marehemu imeagwa mchana huu wa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi kibirizi tayari kwa mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya alihudhuria
katika shughuli hiyo ya kuwaaga marehemu wanjani hapo na kutoa salamu za
rambi rambi kwa ndugu na jamaa za wafiwa.
Kwa upande wake, Katibu wa Bakwata mkoa wa Kigoma, Shekhe Moshi
Guoguo alitoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na Taifa kwa ujumla,
aliwataka waombolezaji kuwa wapole na wavumilivu hasa katika wakati huu
mgumu wa majonzi ya kupotelewa na ndugu zao wapendwa.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA. JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!
CHANZO: MICHUZI BLOG

Note: Only a member of this blog may post a comment.