Kufuatia wadau mbalimbali kuhoji kwa nini staa wa filamu Bongo, Jacob Steven ‘JB’ ameliacha kaburi la aliyekuwa mwongozaji wa filamu katika kampuni yake, marehemu Adam Kuambiana mwenyewe amefunguka kwamba hali ya kifedha ni ngumu kwa sasa.
Akiongea na gazeti la Amani, JB alisema anatamani kulikarabati kaburi la Kuambiana ambalo limetoboka na mpango huo upo kwenye ratiba yake ila kwa sasa hali ya kifedha ni ngumu ikiwa nzuri ataanza ujenzi wake mara moja.
“Unajua ni muda mrefu nilikuwa safarini Mwanza, sasa nimerudi nitafanya mchakato hali ya kifedha ikiwa nzuri nitalijengea kaburi hilo maana nimekuwa nikiulizwa sana kuhusu hili lakini itambulike kwamba Kuambiana alikuwa ni kama mdogo wangu wa damu hivyo lazima nilijengee,” alisema JB.


Note: Only a member of this blog may post a comment.