Sunday, April 12, 2015

Anonymous

Islamic State waharibu vibaya mji wa Nimrod

 Mwanamgambo wa Islamic State akiharibu sanamu
Wanamgambo wa Islamic State wametoa kanda ya video kupitia kwa mtandao ikiwaonyesha wakiharibu maeneo ya thamani kubwa kwenye mji wa Nimrod nchini Iraq.

Picha za wanamgambo hao wakitumia misumeno ya umeme kukata sanamu, zinaonekana kuthibitisha ripoti za mwezi uliopita kutoka kwa maafisa nchini Iraq kuwa wanamgambo hao wameharibu mji wa kitamadanu wa Nimrod.
Wanamgambo hao hutumia tinga tinga na milipuko kuharibu mji huo ambao wakati mmoja ulikuwa ni mji mkuu wa himaya ya Assyrian.
-via BBC SWAHILI

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.