Monday, April 27, 2015

Anonymous

FIFA yamuondoa kocha Simba SC

Mohammed Mdose, Dar es Salaam.
WIKI mbili zilizopita, Simba ilimleta nchini mkufunzi wa makipa anayetambulika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutoka nchini Oman, Haroun Amour, kuwanoa makipa wake kwa muda wa wiki tatu, lakini Fifa imemuondoa akiwa amekaa kwenye timu hiyo kwa wiki moja tu.

Amour, alitua Simba Aprili 14, mwaka huu na kuanza kazi siku hiyohiyo kwenye mazoezi ya timu hiyo katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), lakini akalazimika kuondoka Aprili 22, mwaka huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Amour alisema kuwa amelazimika kukatisha programu aliyoipanga kuwapa makipa wa Simba baada ya kupokea barua ya ghafla kutoka Fifa ikimtaka mara moja aende nchini Bruney kutoa mafunzo kwa makocha wa makipa wa nchi hiyo.

Alisema japokuwa amekaa Simba kwa wiki moja, anaamini kuna vitu vya kiufundi amewapa makipa hao lakini pia ameahidi kurudi mwezi Juni, kwa ajili ya kuwapa mafunzo ziadi yatakayowasaidia msimu ujao.

“Fifa wamenitumia barua ya kunitaka niende nchini Bruney kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa makocha wa nchi hiyo. Japo sijakamilisha programu yangu, sina budi lazima niende kwa kuwa hao ndiyo mabosi wangu,” alisema Haroun.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.