Nimefikiwa
na hii story kutoka Kenya, inahusu mgogoro wa mapenzi kati ya mwanaume
na mwanamke.. chanzo cha ugomvi hakijafahamika, jamaa alifika kwenye
duka hilo, wakajibizana na mwanamke huyo, mwisho wa mzozo jamaa
akammwagia mwanamke petrol, akajimwagia na yeye mwenyewe alafu akawasha
moto ambao uliteketeza jengo la gorofa lililopo Kericho.
Mwanamke huyo alifariki hapohapo, huyo jamaa alipata majeraha makubwa pamoja na watu wengine wanne walijeruhiwa pia..“Akaanza kuwasukuma wateja waliokuwa katika M-Pesa akawaambia wacha nihudumiwe ndio akawasha kiberiti“, alisema shuhuda mmoja aliyekuwa eneo hilo pia.
Maduka yaliyopo kwenye jengo hilo
yaliwaka moto, ikabidi vikosi vya zimamoto kufika ili kuuzima moto huo
ambao tayari ulikuwa umeathiri sehemu kubwa ya jengo hilo.
Hii ishu ilikuwa kubwa sana, unaweza kuona hapa hali ilivyokuwa baada ya moto huo kuwashwa..


Note: Only a member of this blog may post a comment.