
Mtanange huo ulitarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi iliyopita lakini kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya baada ya maji kujaa uwanjani mchezo uliahirishwa.
Simba SC imejipatia bao la kwanza kipindi cha pili katika dakika ya 52 kupitia kwa mchezaji wake Ramadhani Singano,dakika ya 64 Kagera Sugar wakasawazisha bao kupitia kwa mchezaji wake Rashid Mandawa lakini dakika ya 68 Ibrahimu Hatibu akaipatia Simba bao la pili kwa njia ya penati.
Mchezo umeisha Kagera Sugar wanaonesha kutoridhika na matokeo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.